Tetesi za Mastaa Ulaya: Ronaldo kutua PSG 2022, Coutinho kurejea EPL

445

Manchester City wanaandaa kiasi cha pauni milioni 127 kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa England na Tottenham Hotspur Harry Kane 28.

Hatima ya Kane itajulikana vyema wiki ijayo baada ya mchezo baina ya City na Spurs wikiendi hii.

Paris St-Germain wanataka kumsajili staa wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo 36, kama mbadala wa Kylian Mbappe 22, ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na miamba ya soka la Hispania Real Madrid msimu wa usajili mwaka 2022.

Kiungo mshambuliaji wa Fc Barcelona Philippe Coutinho, 29, amekuwa akiwindwa na klabu mbalimbali Ulaya ikiwemo Leicester City, Manchester United na Arsenal zote za England ikiwa ni baada ya miaka miwili tangia kutoka Liverpool kwa dau la pauni milioni 142.

Author: Asifiwe Mbembela