Tetesi za Mastaa Ulaya: Salah awekwa mbadala wa Mbappe Madrid, Arsenal yajitutumua kwa Tammy Abraham

Tottenham wanaweza kumsajili kiungo mshambuliaji wa Italia na AS Roma Lorenzo Pellegrini, 25, lakini watalazimika kutoa kiasi cha pauni milioni 26 kwa mchezaji huyo.
Arsenal wanavutiwa kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham 23, ambaye amekosa namba ya moja kwa moja ndani ya The Blues chini ya Thomas Tuchel, Tottenham na Inter Milan zinahitaji huduma yake pia.
Chelsea wanaendelea kumfukuzia mshambuliaji wa kimataifa wa England na Tottenham Hotspur Harry Kane 27, na yule wa Inter Milan Romelu Lukaku 28.
Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti anahitaji klabu hiyo kumsajili winga wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri Mohamed Salah 29, kama dili la kumpata Kylian Mbappe litashindikana.
Mabingwa wa La Liga Atletico Madrid wameonyesha nia ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa England na Manchester United Jesse Lingard, 28, ambaye anahitajika pia na West Ham United.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares