Tetesi za Mastaa Ulaya: Samuel Umtiti kutua Arsenal au Manchester United, Barca yashusha bei yake washindwe wenyewe, Ole Gunnar Solskjaer anamtamani Koulibaly

Barcelona wameshusha bei ya kumuuza mlinzi wa Ufaransa Samuel Umtiti, 26, ambapo hivi sasa anapatikana kwa dau la £27m, vilabu vya Manchester United na Arsenal ni miongoni mwa timu zinazowania saini ya beki huyo.

United wanafikiria kumsajili mlinzi mwingine katika kikosi hicho majira ya kiangazi ambapo kocha mkuu wa timu hiyo Ole Gunnar Solskjaer anamtamani beki wa Senegal na Napoli Kalidou Koulibaly, 28.

Kiungo mshambuliaji wa Juventus na Bosnia-Herzegovina Miralem Pjanic, 30, huenda akapiga chini ofa za kujiunga na klabu za England na kusalia pale pale Turin, Chelsea ilikuwa inahitaji saini yake.

Real Madrid na Manchester United wanaweza kulazimika kusubiri miaka miwili ili kumsajili mshambuliaji wa Borrusia Dortmund Erling Haaland, 19, ambapo strika huyo ana kipengele cha kuondoka klabuni mwaka 2022 kwa dau la Euro 75.

Arsenal wamepanga kumsaini mlinzi wa Borrusia Dortmund Manuel Akanji, 24, kwa dau la £25m, mazungumzo ya kukamilisha dili hilo yalishindikana mwezi Januari, yamefufuliwa hivi sasa.

Hata hivyo, the Gunners wanatazamia kuipiku Everton katika kuipata saini ya kiungo wa Juventus Mfaransa Adrien Rabiot 25, ambapo Arsenal wanadhani anaweza fanya vizuri akishirikiana na Matteo Guendouzi, 21.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends