Tetesi za Mastaa Ulaya: Sancho atengewa donge nono akibakia Dortmund, Arturo Vidal anukia Newcastle United

45

Borussia Dortmund wanakusudia kumuongezea kijana wao Jadon Sancho, 20, Euro milioni 4 (£3.5) kama atazipiga chini ofa mbalimbali kutoka England, kumbuka ahusishwa na Manchester United, Chelsea na Liverpool.

Newcastle wanaweza kumvuta kiungo mkabaji wa Barcelona na Chile Arturo Vidal, 32, kwa sharti moja tu kama watamchukua kocha Max Allegri na kumuacha zao la Steve Bruce.

Mlinzi wa Kihispania Pablo Mari, 26, anayekipiga Arsenal kwa mkopo amesema anataka abakie moja kwa moja hapo asirudi katika klabu mama ya Flamengo.

Virusi vya Corona vitapelekea angauko la bei za wachezaji huku dau la mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa Kylian Mbappe, 21, likishuka mpaka Euro milioni 35-40.

Arsenal wamefanya mawasiliano na mlinzi wa kati wa Reims ya Ufaransa Axel Disasi, 22 kwa lengo la kumvuta Emirates.

Liverpool wameonyesha nia ya kumhitaji kiungo mshambuliaji wa Croatia na Inter Milan Marcelo Brozovic, 27

Lakini bado Liverpool hawajafanya mawasiliano ya awamu ya pili ya kumhitaji strika wa RB Leipzig Timo Werner, 24.

Barcelona wanataka kushinikiza kumuuza winga wa Kibrazil Philippe Coutinho ambaye hivi sasa yuko kwa mkopo Bayern Munich wakivilenga zaidi kwa vilabu vya England kumchukua.

Liverpool wamekusudia kushusha zaidi dau la kumuuza winga wake Xherdan Shaqiri, 28, kwa sababu ya virusi vya Corona.

Author: Bruce Amani