Tetesi za Mastaa Ulaya: Sane, Havertz kutua Bayern Munich, Niguez katika rada za Manchester United

Bayern Munich wanahitaji kumsajili winga wa Manchester City Leroy Sane 24, na Kai Havertz, 20, kutokea Bayer Leverkusen katika ungwe mpya ya kuijenga Bayern Munich ameyasema hayo Mwenyekiti Karl Heinz Rummenige.

Chelsea wanaongoza mbio za kunasa saini ya mlinzi wa pembeni wa Porto Alex Telles huku Paris St-Germain wakifuatia katika rada za klabu.

Mshambuliaji wa RB Leipzig anayewindwa na Liverpool Timo Werner ameweka wazi kuwa anatamani kwenda Liverpool kuliko Inter Milan, hata hivyo Mkurugenzi wa michezo wa Inter Milan amesema hawawezi kumsajili.

Arsenal wanavutiwa kumsajili strika wa Napoli Arkadiusz Milik, 26, lakini watakutana na ushindani kutoka kwa Juventus ambao nao wanahitaji saini ya mshambuliaji huyo.

Manchester United wanaamini kuwa wakala wa Paul Pogba 27, ndiye anashinikiza kiungo huyo kuondoka klabuni mwishoni mwa msimu huu. Paul Pogba amekuwa akihusishwa kujiunga na Juventus na Real Madrid.

Kiungo wa Liverpool Harvey Elliott amepiga chini ofa ya kusajiliwa na Real Madrid, kiungo huyo alikaribishwa na mlinzi wa kati wa Madrid Sergio Ramos ili kurahisisha usajili wake.

Barcelona wamepanga kuendelea kumtoa kwa mkopo kiungo mshambuliaji wao raia wa Brazili Phillipo Coutinho 27, lakini wanahitaji £9m katika klabu inayomhitaji kutokea EPL.

Kiungo wa Atletico Madrid anayewindwa na Manchester United Saul Niguez amesema ataiweka bayana klabu atakayoichezea msimu ujao ndani ya siku tatu zijazo, kiungo huyo wa Hispania ana kipengele kinachomruhusu kuondoka klabuni hapo kwa dau la £130m.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends