Tetesi za Mastaa Ulaya: Tammy Abraham asita kuongeza kandarasi Chelsea kufuatia tetesi kuwa wanamsaka mshambuliaji mpya

139

Manchester United wanahitajika kutoa pauni milioni 68 ili kupata saini ya beki wa kati wa Sevilla na Ufaransa mwenye umri wa miaka 22 Jules Kounde.

Manchester City wanatafakari uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 20, kwa kumtengea kiasi cha pauni milioni 100.

Mshambuliaji zao la Chelsea na England Tammy Abraham, 23, hayuko tayari kuanza kufanya mazungumzo ya kuongezewa mkataba mpya klabuni hapo wakati The Blues wanataka kumsajili strika matata wa Dortmund Haaland.

Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amekiri kuwa kwenye mawasiliano ya karibu na mshambuliaji wa Norwei Erling Braut Haaland tangia akiwa katika klabu ya Molde.

Author: Bruce Amani