Tetesi za Mastaa Ulaya: Willian akataa kubakia Arsenal, Barca kumrudisha Xavi Camp Nou

Baada ya kuonyesha kiwango bora msimu huu kiungo mshambuliaji raia wa Ubeligiji Youri Tielemans, 24, imeelezwa kuwa ataketi kitako na mabosi wa Leicester City kwa ajili ya kumpa kandarasi mpya ya kuendelea kukitumikia kikosi hicho kwa misimu mengine mbeleni.

Winga wa Kibrazil Willian, 32, anayekipiga klabuni Arsenal akitokea Chelsea amepanga kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu lakini hakuna ofa yoyote ambayo imepokelewa na The Gunners.

Kocha wa zamani wa Juventus Massimiliano Allegri inaelezwa kuwa yuko mbioni kujiunga na kikosi cha Real Madrid kurithi mikoba ya Zinedine Zidane Zizzou ambaye anaonekana kuondoka klabuni hapo baada ya Ligi kumalizika.

Barcelona wamefungua mazungumzo na kiungo wao wa zamani Xavi ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha klabu Al Sadd ya nchini Qatar kuchukua nafasi ya kocha Ronald Koeman.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends