Tetesi za Mastaa Ulaya: Zinedine afanya mazungumzo na Man United, Sterling ataka mkopo Barcelona

Manchester United wanaendelea na majaribio ya kumsajili kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane kwa ajili ya kuichukua timu hiyo kurithi mikoba ya Ole Gunnar Solskjaer.

Winga wa Manchester City na England Raheem Sterling ameiomba klabu yake imtoe kwa mkopo kwenda Fc Barcelona katika dirisha dogo la Januari, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, ameanza mechi tatu msimu huu.

Arsenal wanakaribia kumsajili mshambuliaji kinda wa RB Salzburg looking to sign RB Salzburg Karim Adeyemi, 19, raia huyo wa Ujerumani anatazamiwa kama mbadala wa Alexandre Lacazette.

Manchester United wanavutiwa kumsajili winga wa kimataifa wa Ufaransa na Fc Barcelona Ousmane Dembele 24, ambapo mchezaji huyo anaweza kuondoka kwani anaingia kwenye miezi sita ya mwisho ya mkataba wake.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends