Tetesi za Soka Ulaya: United yamganda Pogba, Virusi vya Corona vyanufaisha vilabu

Kwenye kipindi hiki ambacho ugonjwa wa Corona unaendelea kusambaa katika maeneo mengi duniani huku katika masuala ya michezo mbalimbali imesimamishwa kutoka na hofu hiyo kilichobaki ni vilabu kuendeleza mawindo ya wachezaji wapya.

Hapa Amani Sports News inakuletea baadhi ya tetesi za soka zinazozungumzwa zaidi duniani tukielekea katika dirisha kubwa la usajili.

Klabu ya Manchester United iko katika mazungumzo ya kumuongezea mkataba kiungo ghali wa timu hiyo Paul Pogba ambaye mkataba wake una malizika katikati ya mwezi Juni 2021. Pogba 27, amekuwa akihusishwa kujiunga na Real Madrid na Juventus.

Mbali na Pogba, United inategemea kumbakiza straika ingizo jipya Odion Ighalo, 30, ambaye amefanya vizuri tangu aingie klabuni hapo kwenye dirisha dogo la Januari.

Juventus inajiandaa kuwasilisha ofa ya kumuongezea mkataba mshambuliaji wake raia wa Ureno Cristiano Ronaldo, 35, mkataba ambao utarefusha uwepo wake katika klabu hiyo ya Italia hadi mwaka 2024.

Mshambuliaji wa England na Tottenham Harry Kane, 26, akapiga chini dili la uhamisho wa fedha nyingi wa kwenda Manchester United au Manchester City na badala yake kujiunga na Juventus.

Manchester City wanatumia muda uliowekwa wa kuahirisha ligi ya Primia kujadili mkataba mpya wa wachezaji Kevin De Bruyne, 28, na Raheem Sterling, 25.

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta anamtaka beki wa West Ham ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa £60m Issa Diop, 23, ambaye pia ananyatiwa na Manchester United.

Kinda wa Birmingham City Jude Bellingham anakabiliwa na kibarua kigumu cha kuamua ahamie wapi kati ya klabu nne zinazomtaka- Manchester United, Chelsea, Bayern Munich and Borussia Dortmund – ambao wako tayari kulipa £30m kumpata Muingereza huyo wa miaka 16.

Barcelona, Manchester United na Real Madrid zitamenyana kumpata kiungo wa kati wa Fenerbahce Mturuki Omer Beyaz, 16.

Mlinda mlango wa mkopo wa Sheffield United Dean Henderson, 23, anatarajiwa kurejea katika klabu yake ya Manchester United msimu wa joto licha ya Chelsea kuonesha nia ya kutaka kumnunua.

Tottenham imekuwa ikimnyatia kiungo wa kati mshambulizi wa Queens Park Rangers (QPR) Eberechi Eze, 21, huku klabu hiyo ya Loftus Road ikitarajiwa kuitisha £20m kumuachilia kiungo huyo wa chini ya miaka 21.

Mashabiki wametoa wito kwa wamiliki wa West Ham, David Sullivan na David Gold kuuza klabu hiyo licha ya ongezeko la kutoridhishwa kwao na utendaji kazi wake.

Klabu kadhaa za Ulaya zilizo na wachezaji wa hadhi ya juu waliojeruhiwa huenda zikafaidi mapumziko yaliyotokana mlipuko wa Corona, miongoni mwa klabu hizo ni Real Madrid iliyo na Eden Hazard, Manchester United yenye Paul Pogba, Barcelona yenye Dembele na Liverpool yenye Allison Becker.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares