Tetesi za usajili Ulaya: Mkhitaryan kubakia Roma, Xavi sasa kurejea La Liga

Karibu katika taarifa mbalimbali zinazohusu tetesi za usajili barani Ulaya katika kipindi hiki ambacho dunia inatumia nguvu kubwa kukabiliana na virusi vya Corona, Amani Sports News inakuletea tetesi za usajili barani Ulaya siku ya leo Jumatatu, Marchi 30, 2020.

Real Madrid wanavutiwa kumsajili mshambuliaji wa Gabon na klabu ya Arsenal Pierre Emerick Aubameyang, 30, licha ya mpango huo utatokea kama wakimkosa kinda wa Borrusia Dortumund Erling Braut Haaland, 19.

Real wanahitaji pia kumnasa kiungo Igor Gomes, 21 raia wa Brazil kutoka Sao Paolo kwa dau la pauni milioni 45.

Newcastle United wanasubiri mwishoni mwa msimu huu kuwavuta wachezaji wawili wa Burnley Robbie Brady na Jeff Hendrick, wote 28, kama wachezaji huru. Raia hao wa Jamhuri ya Ireland mikataba yao inatamatika mwishoni mwa msimu huu Turf Moor.

Kiungo wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan anategemea kubakia moja kwa moja katika klabu ya Roma mwishoni mwa msimu huu. Arsenal inahitaji £18 ingawa Roma wapo tayari kutoa £10 pekee.

Kiungo wa zamani wa Barcelona na Hispania Xavi amesema yuko tayari kuinoa timu yoyote ndani ya La Liga kama itatokea fursa hiyo, saa hizi niko tayari na naweza kutawala vyema vyumba vya kubadilishia nguo.

Mlinda mlango wa Aston Villa Tom Heaton, 33, anahitaji kwenda kusomea ukocha baada ya kumaliza kutoa huduma ya mpira, huenda atarudi Burnley katika klabu ya utotoni mwake.

Everton wanaendeleza matumaini ya kufanikiwa kupata ruhusa ya kujenga uwanja wao mpya licha ya uwepo wa janga la virusi vya Corona.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends