Tetesi za usajili Ulaya: Harry Kane apishana na Man United, Jesus aingia njia za Madrid

Karibu katika taarifa mbalimbali zinazohusu tetesi za usajili barani Ulaya katika kipindi hiki ambacho duniani inatumia nguvu kubwa kukabiliana na virusi vya Corona, Amani Sports News inakuletea tetesi za usajili barani Ulaya siku ya leo Jumapili, Aprili 5, 2020.

Real Madrid wamepanda kupotezea ombi la Manchester City juu ya kumhitaji mlinzi wa Kifaransa Raphael Varane, 26. Valane amekuwa katika kiwango kwa muda sasa tangu alipoaminiwa klabuni hapo.
Miamba ya Italia Juventus imejiandaa kumtoa kafara winga wake Douglas Costa, 29, kwenda Manchester City ili iwe sehemu ya ushawishi wa kumnasa strika wa City kutoka Brazil Gabriel Jesus, 23.
Huenda Liverpool watamuachia kinda wao Rhian Brewster, 20, kwenda kwa mkopo kwingineko endapo wakifanikiwa kumpata mshambuliaji wa Kijerumani na RB Leipzig Timo Werner, 24.
Celtic wanahaha kumbakiza mlinzi wao raia wa Norwei kipindi hiki ambacho AC Milan wameeonyesha nia ya kumhitaji katika majira ya kiangazi.
Bosi wa Everton Carlo Ancelotti ameanzisha mpango kazi wa kumshawishi kiungo Gareth Bale, 30, na James Rodriguez, 28, wote kutoka Real Madrid na wamekosa nafasi ndani ya Bernabeu.
Chelsea wako kwenye makubaliano na Philippe Coutinho, 27, ambaye hivi sasa yupo kwa mkopo Bayern Munich akitokea FC Barcelona.
Wakati huo huo, Chelsea wapo kwenye mazungumzo ya kumshawishi Achraf Hakimi wa Borrusia Dortmund ambaye hivi sasa anahusishwa na Paris Saint Germain.
Manchester United wameambiwa hakuna uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa wa Tottenham na England Harry Kane, 26, kutokana na urefu wa mkataba wa strika huyo.
Mlinzi Matthijs de Ligt, 20,  ameingia kwenye rada ya Manchester United katika kipindi hiki ambacho mlinzi huyo bado hajajihakikishia namba Juventus.
Newcastle United hawajakata tamaa bado ya kuwania saini ya kiungo anayetajwa kuwa bora wa Lille Boubakary Soumare, 21, licha ya kuwa kwenye mazungumzo na Real Madrid pia.
Liverpool wanahusishwa pia  kumsajili Soumare na wapo kwenye mazungumzo ya awali.

Author: Bruce Amani