Tetesi za usajili Ulaya: Ighalo atengewa mamilioni Shanghai kuitema United

Karibu katika taarifa mbalimbali zinazohusu tetesi za usajili barani Ulaya katika kipindi hiki ambacho duniani inatumia nguvu kubwa kukabiliana na virusi vya Corona, Amani Sports News inakuletea tetesi za usajili barani Ulaya siku ya leo Ijumaa, Marchi 27, 2020.

Mabingwa mara nyingi zaidi wa Uefa 13 Real Madrid wanavutiwa kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 19, katika majira ya kiangazi. Kinda huyo raia wa Norwei amejiunga na Dortmund msimu huu na ana kipengele cha kuondoka klabuni hapo kwa dau la £50, gazeti la Standard limeripoti.

EFL imeviambia vilabu kuwa michezo haitarejea Aprili 30 kama ilivyopangwa hapo awali badala yake tarehe ya kurejea kwa ligi itatangazwa wiki lijalo, Mail limeripoti.

Strika anayekipiga kwa mkopo Manchester United Odion Ighalo, 30, amepewa ofa ya mshahara wa zaidi ya £400,000 kwa wiki na klabu yake mama ya Shanghai Shenhua ya China ambako ndiko alikotokea wakati anajiunga na United, Sky Sports limeripoti.

Manchester United wanafikiria kumuongezea makataba kiungo Paul Pogba, 27, lakini hiyo itakuwa ‘chukizo’ kwa mshindi huyo wa Kombe la Dunia, AS limeripoti.

Kiungo mshambuliaji Pedro, 32, amesema ataondoka Chelsea mwishoni mwa msimu huu pale mkataba wake utakapomalizika ndani ya The Blues, Independent limeripoti.

Everton ni miongoni mwa vilabu vinne ambavyo vipo kumshawishi mlinzi wa Lille na Brazil Gabriel, 23, ambaye anatajwa kuwa na thamani ya £30m, gazeti la Sky Spors limeripoti

Barcelona wanataka kumsajili kiungo ghali wa Tottenham Tanguy Ndombele, 23, ambaye alijiunga na Spurs kwa dau la £55m kutoka Lyon majira ya kiangazi ya msimu uliopita,  gazeti la Mundo Deportivo limeripoti.

Tottenham wamefungua mazungumzo na kiungo wa Kiingereza Oliver Skipp, 19, juu ya kumuongezea kandarasi mpya, gazeti la Football Insider limeripoti.

Chelsea, Real Madrid, Barcelona na Bayern Munich wamekuwa wakimtazama kiungo wa Espanyol na Hispania Nico Melamed, 18, ambaye anaweza kuuzwa kwa £7.3m, gazeti la Gianluca Di Marzio limeripoti.

West Ham, Sporting Lisbon na Anderlecht wanamtazamia mlinda mlango wa Liverpool ambaye yupo kwa mkopo Besiktas among Loris Karius, 26, anaweza kupatikana kwa £4.5m mwishoni mwa msimu huu, Voetbal24 wameripoti.

Arsenal wako vitani kusaka saini ya kiungo wa Valencia Carlos Soler, 23, ambapo timu hiyo inahitaji kuwauza wachezaji kuleta uwiano kwenye daftari lao, Sky Sports limeripoti.

Author: Bruce Amani