Tetesi za usajili ulaya: James Rodriguez awaniwa na Everton

Karibu katika taarifa mbalimbali zinazohusu tetesi za usajili barani Ulaya katika kipindi hiki ambacho duniani inatumia nguvu kubwa kukabiliana na virusi vya Corona, Amani Sports News inakuletea tetesi za usajili barani Ulaya siku ya leo Alhamisi Aprili 2, 2020.

West Ham wanajiandaa kuishangaza Barcelona kwa kumhitaji straika aliyejiunga na timu hiyo kwa usajili maalumu Martin Braithwaite, 28, kwa dau la pauni milioni 15, mshambuliaji huyo amecheza mechi tatu pekee.

Borussia Dortmund wako mbioni kushinda mbio za kunasa saini ya kinda anayetajwa kuwa na kipaji kikubwa Jude Bellingham kutoka Birmingham City baada ya Manchester United kujitoa katika mbio hizo.

Straika wa England Marcus Rashford amekiri kuwa anatamani kucheza na fowadi mweza katika kikosi cha England ambaye hivi sasa anakipiga kunako Borrusia Dortmund Jadon Sancho ndani ya Manchester United msimu ujao.

​Manchester United wanatazamia kumsajili mlinzi wa PSG na Ubeligiji Thomas Meunier, 28, ambapo saizi maisha ya baadae ya mlinzi huyo hayajulikani ndani ya uzi wa matajiri PSG.

Meneja wa Everton Carlo Ancelotti anamuangalia fowadi wa Real Madrid James Rodriguez, 28 kama ingizo jipya kwa msimu ujao ndani ya Everton, hao wawili wamewai kuwa pamoja katika kikosi cha Real Madrid.

Willian wa Chelsea amesema anafikiri Liverpool ni timu bora kuliko nyingine EPL hasa ukitazama msimamo wa ligi huku wakiwa hawajabidilisha mwalimu tangu 2015.

Katika hatua nyingine, Willian, 31, huenda akaungana tena na Meneja Maurizio Sarri ndani ya Juventus baada ya wawili hao kufanya kazi pamoja Stamford Bridge siku za nyuma.

Unaweza kusema ni maajabu lakini ndio hivyo tena, mlinzi wa pembeni wa Sheffield Wednesday Morgan Fox, 26, anavutiwa na Middlesbrough timu inayoshiriki ligi daraja la kwanza.

Mlinda mlango wa Leeds United Illan Meslier, 20, anayekipiga kwa mkopo klabuni hapo huenda akabakizwa moja kwa moja endapo timu hiyo itafuzu kucheza EPL kutoka daraja la kwanza, kumbuka Meslier alitokea Ligue 1 katika klabu ya Lorient kabla ya kujiunga na Leeds

Author: Bruce Amani