Tetesi za Usajili Ulaya: Koulibaly, Laporte wazigonganisha Man City, Barca

Karibu katika taarifa mbalimbali zinazohusu tetesi za usajili barani Ulaya katika kipindi hiki ambacho duniani inatumia nguvu kubwa kukabiliana na virusi vya Corona, Amani Sports News inakuletea tetesi za usajili barani Ulaya siku ya leo Jumatatu.

Barcelona wanavutiwa na usajili wa majira ya kiangazi ya mlinzi wa Manchester City na Ufaransa Aymeric Laporte, 25, limeripoti gazeti la Mundo Deportivo la Hispania.

Paris St-Germain, Real Madrid na Manchester City ziko vitani kuwania saini ya mlinzi wa Slovakia na klabu ya Inter Milan Milan Skriniar, 25, hiyo ni kwa mjibu wa gazeti la Calciomercato Italia.

Kalidou Koulibaly, 28, yuko tayari kuondoka Napoli msimu wa majira ya kiangazi, Manchester United wamehusishwa na mlinzi huyo raia wa Senegal, gazeti la Mirror limeripoti.

Kushindwa kwa Barcelona katika kusaka vipaji kumeendelea kuwatesa ambapo sasa wapo tayari kumuachia strika wa Ufaransa Antoine Griezmann kwa Euro milioni 100 mwaka mmoja tangu ajiunge nayo akitokea Atletico Madrid kwa Euro milioni 120, Sport limeripoti.

Liverpool na Arsenal walikuwa wanamchunguza kwa makini kinda wa Eintracht Frankfurt na Ufaransa Evan Ndicka, 20, kabla ya ligi kusimamishwa ili waweze kumsajili kiangazi, Sky Sports limeripoti.

Majanga Barcelona ipo kwenye majadiliano na wachezaji wakubwa klabuni kwa ajili ya kupunguza mishahara yao, klabu imeona haitaweza kuwalipa mishahara yao mpaka mwisho wa ligi ambapo hivi bajeti yao inazidi Euro bilioni 1, gazeti la Marca.

Strika wa Juventus ya Italia Gonzalo Higuain, 32, amevunja kanuni za kutengwa kwa sababu ya hofu ya virusi vya Corona ambapo amesafiri kwenda Argentina kumuangalia Mama yake anayesumbuliwa na Kansa, Sun limeripoti.

Baba wa mshambuliaji wa Real Madrid Luka Jovic, 22, lazima atakutwa na adhabu hata ya kufungwa jela endapo ataamua kuvunja kanuni za kutengwa kwa kwenda kumtembelea mpenzi wake Belgrade, Marca limeripoti.

Kiungo wa zamani wa Arsenal na Barcelona Alexander Hleb amesema hakuna “anayehofu kuhusu Corona” nyumbani kwao Belarus kwani mpaka sasa Ligi kuu nchini humo inaendelea kama kawaida, Sun limeripoti.

West Ham watakumbana na changamoto ya kutumia uwanja wa London kutoka kwa wanariadha wa Uingereza ambao nao wataanza kuutumia katikati ya mwezi Juni, kumbuka uwanja huo hutumiwa kwa kukodiwa, changamoto hiyo itatokea endapo EPL itaendelea mpaka mwishoni mwa mwezi wa sita (Juni), limeripoti gazeti la Times

Author: Bruce Amani

Facebook Comments