Tetesi za usajili Ulaya: Liverpool yamkataa Coutinho, Willian awindwa na Arsenal

922

Karibu katika taarifa mbalimbali zinazohusu tetesi za usajili barani Ulaya katika kipindi hiki ambacho duniani inatumia nguvu kubwa kukabiliana na virusi vya Corona, Amani Sports News inakuletea tetesi za usajili barani Ulaya siku ya leo Jumanne, Marchi 31, 2020.

Manchester United huenda wakabadili gia angani na kuanza kumuwinda kiungo wa Leicester City na England James Maddison, 23, baada ya lengo la kumsajili nahodha wa Aston Villa Jack Glealish, 24, kuota mbawa.

Borussia Dortmund wamesema kinda wake Jadon Sancho, 20, ataigharimu £110 timu yoyote itakayohitaji huduma ya winga huyo, katika kipindi hiki ambacho Manchester United, Chelsea na Liverpool wanawania saini hiyo.

Arsenal, Tottenham Hotspur na West Ham United wanavutiwa kumsajili mlinzi wa Liverpool Dejan Lovren, 30, mlinzi huyo anamaliza kandarasi yake lakini amepoteza hamu ya kusalia klabuni hapo.

Liverpool hawavutiwi tena kumsajili kiungo mshambuliaji wa Brazil Philippe Coutinho ambaye yuko kwa mkopo Bayern Munich kutokea Barcelona.

Manchester United wanaongoza mbio za kunasa saini ya fowadi wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 Coutinho.

Aidha, United wanaamini kuwa kiungo mkabaji raia wa Ufaransa Paul Pogba, 27, ataendelea kusalia klabuni hapo kwa sababu vilabu vingi havitafikia dau la £100m.

Real Madrid wako karibu kukamilisha mazungumzo ya awali kwa kiungo wa Sao Paulo Igor Gomes, 21, wakati ambao Barcelona, Sevilla na Ajax zinavutiwa na Mbrazili huyo.

Winga wa Chelsea na Brazil Willian, 31, anaweza kuendelea kucheza EPL hata akaondoka Chelsea baada ya Arsenal na Tottenham kuonyesha nia ya kumnasa winga huyo.

Kiungo wa Real Madrid Dani Ceballos, 23, anayekipiga Arsenal huenda akarudi Real Betis kama timu yake mama Madrid ikishindwa kumrudisha katika timu hiyo.

Meneja wa Burnley Sean Dyche amesema ni heri msimu huu ukamalizika huku michezo yote ikichezwa bila mashabiki, ‘kama mtindo wa Kombe la Dunia’.

Author: Bruce Amani