Tetesi za Usajili Ulaya: Mabingwa wa Kombe la FA kumpa Aubameyang Mkataba Mpya wiki hii, Man Utd yatamani kuwa na Kasper Schmeichel wa Leicester City

377

Mshindi wa Kombe la FA Arsenal imekusudia kumvuta beki wa kati wa Sevilla Diego Carlos, 27, ambapo kocha Mikel Arteta amepanga kuboresha kikosi chake eneo la ulinzi.

Ripoti nyingine zinaeleza kuwa Arteta anafanya mazungumzo ya chini kwa chini ya kumwania kiungo mshambuliaji wa Barcelona na Croatia Ivan Rakitic, 32, kwa ajili ya kumsajili katika dirisha kubwa la usajili.

Manchester United wanafikiria kumsajili mlinda goli wa Leicester City na Denmark Kasper Schmeichel, 33.

Inaelezwa kuwa Liverpool wamefikia hatua nzuri ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Bayern Munich Thiago Alcantara ambaye anamalizia muda wa mkataba wake, timu ya Paris St-Germain ni miongoni mwa washindani wa Liverpool.

Arsenal watampa mkataba mpya mshambuliaji wake raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 31, kandarasi iliyoboreshwa zaidi yenye thamani ya £250,000 kwa wiki mwishoni mwa wiki hii.

Hata hivyo, Aubameyang anahitaji kuiona Arsenal ikifanya usajili wa majina makubwa ili kuja kutoa ushindini msimu ujao 2020/21.

Winga wa Crystal Palace Winfred Zaha, 27, ni miongoni mwa wachezaji wanaowindwa na mabingwa wa FA Arsenal.

Kocha aliyefungashiwa mizigo katika klabu ya Bournemouth, Eddie Howe amesema atachukua mapumziko ya ukocha kwa kipindi fulani kujiweka sawa.

Author: Asifiwe Mbembela