Tetesi za usajili Ulaya: Man United yaingilia rada za Barca kwa Auba, Neymar kizungumkuti PSG

Karibu katika taarifa mbalimbali zinazohusu tetesi za usajili barani Ulaya katika kipindi hiki ambacho dunia inatumia nguvu kubwa kukabiliana na virusi vya Corona, Amani Sports News itakuwa inakuletea tetesi za usajili barani Ulaya

Mlinda mlango wa Kibrazil Alisson, 27, na mlinzi wa Uholanzi Virgil van Dijk, 28, wapo katika mazungumzo na vinara wa ligi kuu England kwa ajili ya kuongeza mikataba mipya, Goal imeripoti.

Kinda wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 19, atakuwa na mchango mzuri kwenye kikosi cha Chelsea hii ni kwa mujibu wa nahodha wa zamani John Terry, lakini kocha Ole Gunnar Solskjaer wa Manchester United ameonyesha nia ya kumhitaji mchezaji huyo raia wa England, limeripoti gazeti la Evening Standard.

EPL wako kujadiliana juu ya tarehe ya kuanza kwa msimu mpya kipindi ambacho wapo kushinikiza msimu huu 2020/21 umalizike mapema Juni huku ule wa 2021/22 huenda ukaanza Agosti 8, limeripoti gazeti la Telegraph.

Boss wa Everton Carlo Ancelotti anahitaji saini ya strika wa Lazio na timu ya taifa ya Italia Ciro Immobile, 30, imeripoti Goal.

Wawakilishi wa mshambuliaji wa  Paris-St-Germain Neymar, 28, wameiambia Barcelona kuwa staa huyo anataka kuondoka Ufaransa na kurudi Camp Nou, limeripoti gazeti la Star.

Arsenal wanavutiwa na strika wa Burnley Chris Wood, 28, kama mbadala wa mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, kama ataamua kuikacha The Gunners mwishoni mwa msimu huu, Star limeripoti.

Manchester United wanajiandaa kutoa paundi milioni 50 kwa Aubameyang licha ya upinzani kutoka kwa Inter Milan na Fc Barcelona, Metro limeripoti.

Katazo la kutoendelea kwa ligi kumetoa mwanya kwa PSG kuendelea kumshawishi kinda wa klabu hiyo Kylian Mbappe, 21, kuongeza kandarasi mpya, mkataba wake wa sasa unaisha 2022, gazeti la Marca limeripoti.

Manchester United wamefanya kikao cha kujadili uwezekano wa kumsajili kiungo wa Atletico Madrid Thomas Lemar, 24, ambaye awali alikuwa katika rada za Liverpool, Manchester Evening News imeripoti

Author: Bruce Amani

Facebook Comments