Tetesi za Usajili Ulaya: Manchester United kumpeleka Henderson kwa mkopo, Barcelona yawatuliza uepo wa Arsenal kwa Coutinho

392

Liverpool, Everton, Tottenham na West Ham zinavutiwa kumsajili kiungo raia wa Wales David Brooks, 23, baada ya klabu aliyokuwa anaichezea AFC Bournemouth kushuka daraja.

Arsenal wameambiwa wasubili kuanza kwa mazungumzo na miamab ya Spain Barcelona juu ya kumhitaji kiungo wa timu hiyo Philippe Coutinho, 28, anayekipiga kunako klabu ya Bayer Munich kwa mkopo.

Kipa wa Manchester United Dean Henderson, 23, inaonekana atatumia mhula mwingine wa msimu ujao kwa mkopo baada ya kocha wake Ole Gunnar Solskjaer kukiri kuwa itamwia vigumu kuwaridhisha makipa wote watatu kwa kuwapatia nafasi ya kucheza.

Liverpool wamekubali dili la pauni milioni 11.75 kwa ajili ya beki wa kushoto wa Olympiakos ya Ugiriki Kostas Tsimikas, 24, ingawa bado hawajafanya makubaliano ya binafsi mchezaji.

Tsimikas anategemea kusaini kandarasi ya miaka minne yenye thamani ya pauni 50, 000 kwa wiki.

Crystal Palace wameweka pauni milioni 8 kwa timu itakayomhitaji mshambuliaji wao ambaye ni raia wa Ubeligiji Christian Benteke, 29, kwa ajili ya kukuzia pato la klabu hiyo yenye nia ya kumsajili strika wa Watford Ismaila Sarr.

Arsenal wako tayari kupunguza gharama ya pauni milioni 18 kwa Mesut Ozil kama atahitajika na klabu nyingine. Mkataba wa Mjerumani huyo umebakiza mwaka mmoja kutamatika.

Author: Asifiwe Mbembela