Tetesi za usajili Ulaya: Mane kwenye rada za Madrid, Juve yawaruhusu wachezaji kuondoka Italia

Karibu katika taarifa mbalimbali zinazohusu tetesi za usajili barani Ulaya katika kipindi hiki ambacho duniani inatumia nguvu kubwa kukabiliana na virusi vya Corona, Amani Sports News inakuletea tetesi za usajili barani Ulaya siku ya leo Jumatano.

Huenda Sadio Mane, 27, akaikacha Liverpool na kujiunga na Real Madrid wakati kuondoka kwa Strika wa Misri Mohammed Salah, 27, itakuwa vizuri zaidi kwa wachezaji hao, hayo yamesemwa na mchezaji wa zamani wa Liverpool Mohamed Sissoko limeripoti Sun.

Winga wa Manchester City na England Raheem Sterling, 25, bado hajatulia katika kikosi hicho tangu alipoihama Liverpool na kujiunga na matajiri wa City, gazeti la Sky Sports limeripoti.

Liverpool, Manchester City na Arsenal zinavutiwa na mlinzi wa Schalke 04 Malick Thiaw ambaye ana futi 6, raia huyo wa Ujerumani anaweza akaondoka klabuni hapo kwa dau la pauni milioni 6.9, Mail limeripoti.

Hofu ya Manchester United ya kumpoteza kiungo wao na mshindi wa Kombe la Dunia Paul Pogba, 27, imeanza kupotea kutokana na vilabu vingi kuhofia gharama za kumtoa Old Trafford, ESPN imeripoti.

Real Madrid wanataka huduma ya strika matata wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 19, kwenye dirisha kubwa la usajili licha ya raia huyo wa Norwei kuhitajika pia Manchester United na Tottenham, Mundo Deportivo limeripoti.

Chelsea wapo tayari kutoa paundi milioni 23 kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa pembeni wa Getafe Marc Cucurella, 21, katika majira ya kiangazi, Diario Sport la Hispania limeripoti.

The Blues pia wanavutiwa na mlinzi wa Ajax na Argentina Nicolas Tagliafico, 27, baada ya kushindwa kumshawishi Ben Chilwell, Calciomercato limeripoti.

Huenda mlinzi wa Manchester United anayekipiga kwa mkopo Roma Chris Smalling, 30, akasalia moja kwa moja klabuni hapo hiyo itatokea endapo  Mashetani Wekundu hao watamsajili mlinzi wa Senegal Kalidou Koulibaly kutoka Napoli, Gazzeta dello Sport limeripoti.

Borussia Moenchengladbach wamesitisha mazungumzo na Barcelona juu ya kuhitaji huduma ya strika Alassane Plea, 27, gazeti la Sport Bird limeripoti.

Zoezi la kutengwa kwa wachezaji na viongozi wa Juventus linatamatika leo Jumatano ambapo sasa wanaruhusiwa kwenda kwenye mataifa yao mama. Ruhusa hiyo haitawahusu Daniele Rugani, Blaise Matuidi na Paolo Dybala ambao wataendelea kutengwa katika kipindi hiki wanachopatiwa matibabu ya virusi vya Corona, Gazzeta dello Sport limeripoti.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments