Tetesi za usajili Ulaya: Sancho ndani ya United, Adebayor karantini ya Corona

429

Karibu katika taarifa mbalimbali zinazohusu tetesi za usajili barani Ulaya katika kipindi hiki ambacho duniani inatumia nguvu kubwa kukabiliana na virusi vya Corona, Amani Sports News inakuletea tetesi za usajili barani Ulaya siku ya leo Alhamisi.

Mmiliki wa Leeds United Andrea Radrizzani ameweka bayana kuwa alitaka kumsajili mshambuliaji wa PSG Edinson Cavani, 33, na Zlatan Ibrahimovic, 38, ambaye hivi sasa yuko AC Milan katika dirisha dogo la Januari lililopita, gazeti la Mail limeripoti.

Manchester United wanaongoza mbio za kunasa saini ya fowadi wa England na Borussia Dortmund Jadon Sancho, 20, mwezi wa sita dirisha kubwa litakapo funguliwa, Independent limeripoti.

Real Madrid wanakusudia kuishawishi Arsenal kwa kuwapa pesa na mchezaji mmoja ili kumpata strika wa Gabon Pierre Emerick Aubameyang, 30, gazeti la Star limeripoti.

Manchester United wapo tayari kumuachia mlinzi wa England Chris Smalling, 30, kusalia Roma moja kwa moja kama watafanikiwa kupata saini ya mlinzi wa Senegal Kalidou Koulibaly, 28, La Gazzeta dello Sport limeripoti.

Arsenal hawako nyuma kwenye tetesi za usajili,  wamepanga kumsaini mlinzi wa Manchester United Chris Smalling huku United ikihitaji Euro milioni 25, Metro limeripoti.

Beki kisiki wa Tottenham na Ubeligiji Jan Vertonghen, 32, amekiri kutokuwa na uhakika kama atasalia na kuongeza mkataba mpya Spurs kwa msimu ujao, Mirror limeripoti.

Arsenal wanaamini kuwa wataishawishi Real Madrid juu ya kusogeza mbele kwa ukomo wa Dani Ceballos, 23,  kuitumikia timu hiyo, The Gunners wanataka baada ya mkataba wa awali waingie kwenye kandarasi nyingine ya mkopo, Standard limeripoti.

Leicester City wanahusishwa na usajili wa beki wa Atalanta na Ubeligiji Timothy Castagne, 24, Sport Foot, via Leicester Mercury limeripoti.

Timu anayochezea Wayne Rooney Derby County imehusishwa kumtaka kinda wa Fenerbahce Ferdi Kadioglu, 20, Derby Telegraph limeripoti.

West Brom wanataka kumsajili moja kwa moja kiungo raia wa Croatia Filip Krovinovic, 24, baada kumalizika muda wa kucheza kwa mkopo Benfica, Express limeripoti.

Dirisha la usajili la kiangazi huenda likaendelea mpaka mwezi Januari endapo virusi vya Corona vitaendelea kusimamisha kwa michezo ya Ligi Kuu England na EFL, Express limeripoti.

Meya wa Bergamo Giorgio Gori amesema huenda mechi ya Uefa kati ya Atalanta dhidi ya Valencia iliyochezwa Februari 19 katika mji wa Milan ndiyo iliyoeneza zaidi maambukizi ya COVID-19 kwa mataifa mawili Italia na Hispania, Mail limeripoti.

Strika wa zamani wa Arsenal na Tottenham Emmanuel Adebayor, 36, amewekwa karantini jijini Benin kutokana na hofu ya virusi vya Corona. Adebayor alikuwa anasafiri kutoka Paraguay anakocheza soka lake katika klabu ya Olimpia kwenda kwao Togo kuungana na familia yake, lakini amekubwa na kizuizi hicho kitakachomfanya abakie hapo kwa siku 15, Talksport limeripoti.

Viongozi wa soka barani Ulaya wamebakiza matumaini tu wakiamini ligi mbalimbali na michuano mingine barani humo zitamalizika kabla ya tarehe 30 Juni, Sky Sports limeripoti.

Mazungumzo ya kuwaongezea mikataba mipya wachezaji wanne ndani ya Chelsea yamesimama kupisha vita dhidi ya COVID-19. The Blues walikuwa katika mazungumzo na winga Willian 31, Olivier Giroud, 33, Pedro, 32, na Willy Caballero, 38, Telegraph limeripoti.

Barcelona wanafikiria kuwakata mishahara wachezaji wote kwa asilimia 70 kwa muda wote wa virusi vya Corona, Guardian limeripoti.

Vilabu vinane vya EPL vimeafikiana kuwa pamoja ili kuidhibiti Manchester City kushinda kwenye rufaa yao ya kucheza Uefa msimu ujao. Vilabu hivyo vimepanga kuhakikisha City inaendelea na adhabu yake ya matumizi makubwa ya pesa, Times subscription limeripoti.

Author: Bruce Amani