Tetesi za Usajili Ulaya: Willian akubaliana na Arsenal, Lingard awekwa sokoni Manchester United

Klabu ya Arsenal inakaribia kuingia kandarasi mpya ya miaka mitatu na staa wao raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 31, nahodha huyo wa The Gunners amekuwa akihusishwa kujiunga na miamba ya Catalunya FC Barcelona na Inter Milan.

Manchester United wapo tayari kusikilizaji ofa mbalimbali za kumhitaji staa wao Jesse Lingard, 27. Kiungo wa Kihispania na Bayern Munich Thiago Alcantara, 29, anahitaji kuhamia katika klabu bingwa ya England Liverpool, ingawa Liverpool watalazimika kuwauza baadhi ya mastaa ili kupata pesa za kumsajili kiungo huyo.

Liverpool wanaweza kupata ushindani wa kumsajili mlinzi wa Kialgeria Aissa Mandi, 28, West Ham na Fenerbahce ni miongoni mwa timu zinazo hitaji huduma ya beki huyo wa Real Betis ya Hispania.

Edinson Cavani, anauhusishwa kujiunga na Leeds United, Benfica na Inter Miami, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 anaweza pia akajiunga na klabu ya Brazil Atletico MG, aliachana na Paris Saint Germain mwezi Juni.

Lazio wana matumaini ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Manchester City David Silva, 34 mwishoni mwa msimu huu.

Arsenal imekubaliana na winga wa Kibrazil Willian, 31, ambaye anakipiga kunako klabu ya Chelsea mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya £100,000 kwa wiki.

Barcelona wanatafakari kumchukua beki kisiki wa Leicester City na Uturuki  Caglar Soyuncu, 24, kwa dau la pauni milioni 40.

Manchester United ipo tayari kumuuza beki wa Ivory Coast Eric Bailly, 26, ambapo AC Milan imeonyesha nia kumhitaji mlinzi huyo aliyesajiliwa United kipindi cha kocha Jose Mourniho.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends