TFF yaramba dili nono kutoka GSM

Shirikisho la Kandanda Tanzania TFF limeingia kwenye mkataba wa miaka miwili na Kampuni ya GSM Group, mkataba wenye thamani ya bilioni 2.1 kwa ajili ya kuidhamini Ligi Kuu Tanzania Bara.

GSM Group ameingia kwenye huo mkataba kama mdhamini mweza wa Kampuni ya NBC ambayo awali iliingia mkataba na TFF wa miaka mitatu kwa ajili ya kuidhamini Ligi baada ya Kampuni ya simu ya Vodacom kujiondoa.

Mkataba huo, umesainiwa mbele ya Makamu wa kwanza wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani na Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Group, Mhandisi Hersi Said ambapo kwa pamoja wameonyesha mfano wa hundi mbele ya Waandishi wa Habari katika tukio lililofanyika Leo Jumanne Novemba 23, 2021.

Akizungumza kwa niaba ya Rais wa TFF, Makamu Rais Ndg. Nyamlani amesema ni wakati sasa wakuachana na baadhi ya mizaha ambayo haina afya katika soka letu, badala yake tujikite kuhamasisha wadau wengine kuwekeza katika soka.

Kwa upande wake, Hersi Said amesema mbali na kuidhamini Yanga, Coastal Union na Namungo udhamini wa sasa umekuwa bora na wenye lengo la kuona ushindani zaidi kwenye Ligi ilikuwa na ligi bora na baadaye kuwa na timu ya taifa nzuri.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends