TFF yasema uchaguzi wa Yanga utafanyika katika siku saba

156

Kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la Kandanda Tanzania imesema itatangaza tarehe mpya ya uchaguzi wa klabu ya Yanga katika sikui saba sijazo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa kamati hiyo Ally Mchungahela amesema wamefanya uamuzi huo baada ya kupitia taarifa za wanachama waliowasilisha mahakamani na kugundua kuwa hawakuwa hai. Alisema kulikuwa na mwanachama  mmoja tu ambaye ni hai lakini wawili hawakuwa hai kwa hiyo hawakuwa na sifa za kuwasilisha kesi mahakamani

“tumeongea na mwanachama huyo asitishe kesi yake mahakamani” alisema Mchungahela. Ameongeza kuwa katiba ya Yanga, TFF,CAF na hata FIFA haziruhusu wanachama wa vilabu kupeleka kesi mahakamani bali kesi hizo zinapaswa kutatuliwa na shirikisho la kandanda TFF.

Wanachama waliofungua kesi walipinga miongoni mwa mengine uhalali wa kadi za zamani, kukataliwa majina ya baadhi ya wanachama kuingizwa katika kitabu na sintofahamu ya Mwenyekiti wao kiasi kwamba wagombea wengine walishindwa kujitokeza kugombea katika uchaguzi huo.

Author: Bruce Amani