TFF yasitisha uchaguzi mkuu wa Simba

22

Shirikisho la kandanda la Tanzania TFF limesitisha uchaguzi mkuu wa klabu ya Simba kutonkana na mambo kadhaa kutokaa Sawa. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya TFF Revocatus Kuauli amesema mchakato huo wa kitengo cha uchaguzi umegubikwa na mambo mengi ambayo yaameenda kinyume na utaratibu wa uchaguzi

Ameeleza kuwa mojawapo ya mambo hayo ni ada ya uwanachama kwa ngazi ya mwenyekiti pamoja na wajumbe kutofautiana, jambo ambalo ni kinyume na katiba ya TFF pamoja na katiba ya klabu hiyo.

Klabu ya Simba ilitangaza kufanya uchaguzi mkuu Novemba 3, 2018 kuwachagua viongozi mbali mbali ndani ya klabu hiyo baada ya kukamiika mchakato wa kubadilisha katiba na kuingia katika mfumo wa hisa na kuachana na uendeshaji wa mfumo wa kizamani wa kutegemea wanachama

Author: Bruce Amani