TFF yawatetea waamuzi licha ya kuonekana kama wanavurunda

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Wallace Karia amesema hatowachukulia hatua yoyote waamuzi licha ya shinikizo kubwa kutoka kwa wadau na mashabiki wa soka nchini kutaka TFF ichukue hatua dhidi ya waamuzi wanaoonekana kushindwa kutafsiri vyema sheria 17 za mpira wa miguu.
Kauli ya Rais Karia imekuja ikiwa ni siku kadhaa tangu kuibuka malalamiko mengi juu ya uamuzi wa waamuzi kwenye mechi za Ligi kuu ikiwamo ile ya Simba na Polisi, Simba na Namungo, Yanga na Coastal, Simba na Mwadui, Ruvu Shooting V Mtibwa Sugar na Mbeya City na Azam.
“Nataka nipate taarifa ya tatizo ni nini kwa waamuzi wetu, binafsi kama rais wa TFF siwezi kuwachukulia hatua waamuzi, lakini kama mahali kunakohusika wakishindwa kufanya hivyo, mimi nitadili nao,” alisema.
Karia aliongeza kwa kusema, idara ya mashindano ya TFF itakutana na kamati ya waamuzi na Bodi ya Ligi ili kumaliza tatizo hilo haraka iwezekanavyo.
Karia amekiri kuwepo na tatizo kwa baadhi ya waamuzi kwenye soka amekwenda mbali zaidi na kusema hiki kinachoendelea hivi sasa kuhusu waamuzi kinahitaji mjadara mpana.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments