Thomas Tuchel mbioni kutua Stamford Bridge kurithi mikoba ya Frank Lampard

245

Kocha Thomas Tuchel hana kazi kwa hivi sasa tangia afutwe kazi ndani ya Paris St-Germain lakini anatajwa kuwa mbioni kutua ndani ya Stamford Bridge kuchukua mikoba ya kocha Frank Lampard ambaye alifutwa kazi mchana wa siku ya Jumatatu Januari 25, 2021.

Chelsea kumtaja Tuchel wanaamini katika uwezo wa kukitumikia kikosi ambacho kina wachezaji wengi vijana na wenye uwezo mkubwa lakini pia waliosajiliwa kwa pesa kubwa katika dirisha kubwa la usajili la mwezi Juni 2020 baada ya Lampard kushindwa.

Kiuhalisia, Tuchel ni miongoni mwa makocha wagumu barani Ulaya, akiwa katika umri wa miaka 47 tayari amefanya kazi katika mazingira tofauti yaliyompa uzoefu wa kufanya kazi eneo lolote lile, kumbuka kabla ya kutua PSG alifanya kazi Mainz na Borrusia Dortmund ya Ujerumani.

Ni mgumu kwa sababu ya msimamo na imani yake, mwezi Disemba wakati anafutwa kazi PSG moja ya sababu zinazoelezwa ni kushindwa kuelewana na Mkurugenzi wa Michezo ndani ya matajiri wa Jiji la Paris Leonardo.

Ameshafanaya makubwa hana shaka kama ilivyokuwa kwa Lampard katika eneo la ukocha, alibeba mataji mawili mfululizo ya Ligue 1 na kuifikisha fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya PSG licha ya kupoteza.

Tuchel endapo atatua Stamford Bridge anaweza akatengeneza historia kama ya kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ambaye pia alipita Dortmund kama ilivyo kwake na tayari amefanya kazi nzuri lakini pia Pep Guardiola sasa Manchester City ambaye alifanya kazi Bayern Munich wakiwa ni makocha wawili wanaomvutia zaidi.

Author: Bruce Amani