Timu ya Madagascar yazawadiwa kwa kutinga AFCON

Serikali ya Madagascar imeitunuku timu ya taifa ya kandanda ya nchi hiyo kwa kufuzu kwa mara ya kwanza katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.

Timu hiyo maarufu kama Barea ilijikatia tikiti katika tamasha hilo la mwaka ujao nchini Cameroon baada ya kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Equatorial Guinea Jumanne

Kaimu rais wa Madagascar Rivo Rakotovao alikikabidhi kikosi hicho pamoja na benchi la kiufundi dola 28,150 kutokana na juhudi zao.

Taarifa pia imesema wametunukiwa Heshima za Kitaifa kwa mafanikio yao ya kutika hatua ya michuano ya fainali ya AFCON 2019

Madagascar ambayo inaorodheshwa nambari 106 katika viwango vya FIFA ilitoka sare ya 2-2 na Senegal ambayo ilicheza Kombe la Dunia 2018, na kupata ushindi mfululizo dhidi ya Equatorial Guinea na kuwa taifa la 40 tofauti kufuzu katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends