Timu zasubiri droo ya hatua ya 32 bora za Kombe la TFF

58

DROO ya Hatua ya 32 Bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) inatarajiwa kufanyika kesho 5:00 makao makuu ya Azam TV Tabata mjini Dar es Salaam

Kwa mwaka wa pili mfululizo, vigogo wa soka nchini Simba SC wametolewa mapema tu katika hatua ya timu 64 wakifungwa 3-2 na Mashujaa ya Kigoma, inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza Tanzania Bara huku timu zilizofuzu hatua hii ni pamoja na mabingwa watetezi, Mtibwa Sugar, Yanga SC, Azam FC, Lipuli FC, KMC, Coastal Union, Kagera Sugar, Mbeya City, Stand United, JKT Tanzania, Singida United, Alliance FC na African Lyon.

Nyingine ni Biashara United, Boma, Namungo, Mbeya Kwanza, Friends Rangers, Majimaji FC, Dodoma FC, Pamba SC, Rhino Rangers, Reha FC, Dar City, Polisi Tanzania, Mashujaa, Transit Camp, The Mighty Elephant, Cosmopolitan, Kitayosce, La Familia FC na Pan African.

Author: Bruce Amani