Tonombe awapa shangwe Wanayanga, tayari kuwavaa Coastal Union

Uongozi wa Yanga umewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuhusu hali ya kiungo wao, Mukoko Tonombe raia wa Congo ambaye alionekana kuumia kwenye mechi ya Ligi Kuu nchini Tanzania VPL dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo uliomalizika kwa Yanga kushinda bao 1-0.

Kiungo huyo alishindwa kuendelea na mchezo huo uliopigwa baada ya kugongana na mchezaji wa Mtibwa kabla ya kuomba kutolewa.

Tonombe alitolewa nje katika dakika za nyongeza za mchezo huo akiwa amebebwa kwenye machela.

Ofisa Mhamasishaji wa timu hiyo, Antonio Nugaz, amesema kuwa anaendelea vizuri baada ya kushinda kuendelea na mchezo huo.

Nugaz amesema kiungo huyo anaendelea vizuri baada ya kupatiwa huduma ya kwanza na madaktari wa timu hiyo mara baada ya kutolewa nje.

Aliongeza kuwa kiungo huyo yupo chini ya uangalizi huku akiendelea kupatiwa matibabu ya haraka ili kuhakikisha anapona haraka na kurejea uwanjani katika michezo ijayo ya ligi na Kombe la FA.

Tonombe amekuwa mhimili wa klabu ya Yanga katika eneo la kiungo mkabaji hasa baada ya kuondoka kwa Papy Kabamba Tshishimbi.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares