Tottenham Hotspur wakopa pesa Benki Kuu kukabiliana na Covid-19

Klabu ya Tottenham inayoshiriki ligi kuu nchini England imepata mkopo kutoka Benki Kuu ya England kiasi cha £175m ( Tsh 511,484,411,375) fedha itakayotumika kupambania athari za janga la virusi vya Corona.

Spurs wamemesema watapata hasara ya kiasi cha hadi £200m (Tsh 584,662,512,000) kufikia Juni 2021, athari zinazojitokeza kutokana na michezo iliyosalia kuchezwa bila uwepo wa mashabiki na kulipa fidia kwa makampuni ya matangazo ya TV.

Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy alisema “tumekuwa na uendeshaji wa klabu hiyo kwa kuangalia uchumi zaidi hivyo lazima tujipatie fedha za kusaidia timu”

Spurs, ambao wamecheza misimu minne mfululizo ya ligi ya mabingwa Ulaya hivi sasa wanakamata nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi kuu nchini England ambapo pointi saba dhidi ya timu iliyonafasi ya nne Chelsea, mechi tisa zikiwa zimesalia.

Levy, ambaye alichukua nafasi ya Sir Alan Sugar katika nafasi ya Uenyekiti Februari 2001, aliongeza kwa kusema  ” Nilisema Marchi 18 kuwa katika miaka yangu 20 klabuni tumepitia changamoto nyingi lakini hakuna shida ambayo tumewai kupitia katika uongozi wangu inayofikia shida ya janga la virusi vya Corona (Covid-19).

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends