Tottenham Hotspur yatanga-tanga kumpata mrithi wa Mourinho

Klabu ya Tottenham Hotspur imeendelea kusaka mbadala wa kocha Jose Mourinho aliyetimuliwa klabuni hapo mwezi Aprili kufuatia matokeo mabovu kwenye mechi za Ligi Kuu England msimu wa 2020/21.
Katika kuhaha huko, klabu hiyo iko kwenye mazungumzo na aliyekuwa kocha wa AS Roma ya Italia Paulo Fonseca raia wa Ureno ili aje kuwa kocha mpya klabuni hapo.
Spurs bado hawajakubaliana lolote na kocha Fonseca, ingawa mazungumzo yanaendelea ambapo mwanzoni pia walikuwa na mawasiliano na aliyekuwa kocha wa zamani wa Chelsea Antonio Conte ingawa dili hilo halikukamilika.
Fonseca alifanya vizuri ndani ya Roma lakini mabosi wa timu hiyo walimfuta kazi baada ya kumaliza nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu Italia Seria A.
Fonseca alichukua nafasi ya kocha Claudio Ranieri Roma ambapo kabla ya kazi hiyo amewai kufanya kazi kunako klabu ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine, Porto na Braga za Ureno.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares