Tottenham kuwachunguza wachezaji waliovunja kanuni za kujitenga, orodha ya wachezaji waliovunja kanuni hizo hii hapa

Siku za kurejea kwa michezo katika nchi mbalimbali barani Ulaya zinakaribia ambapo kila taifa linapambana kuhakikisha ligi zinachezwa na kumalizika salama.

Lakini wakati ligi zikirejea baada ya takribani miezi miwili ya kutofanyika kwa michezo, wachezaji, makocha, na viongozi katika klabu walitakiwa na mamlaka za ndani ya klabu, wataalamu wa afya pengine mpaka serikali kuwadhibiti wachezaji kutokiuka kanuni za kujitenga.
Licha ya kanuni hizo lakini baadhi ya wachezaji walikiuka. Hapa Amani Sports News inakuletea majina ya wachezaji waliokiuka na kuvunja kanuni za kujitenga.
  • Mlinzi wa Manchester City Kyle Walker alivunja kanuni za kujitenga baada ya kufanya sherehe na mpenzi wake, baada ya hapo akasafiri kwenda kwa wazazi wake Kusini mwa Yorkshire. Baada ya hapo aliwaomba radhi kwa mashabiki wake.
  • Straika wa Everton Moise Kean alikiuka kanuni za kujitenga baada na yeye kuandaa sherehe ndogo ndani ya nyumba yake hata hivyo anasubilia adhabu ya utovu wa nidhamu.
  • Nahodha wa Aston Villa Jack Grealish alipigwa picha akiwa kwenye gari anaelekea kwa kumuona rafiki yake. Aliomba msamaha na kusema ameaibika vya kutosha.
  • Wachezaji wawili wa Tottenham Serge Aurier na Moussa Sissoko walikiuka kanuni kufuatia kufanya mazoezi ya pamoja licha ya kujua ni kosa, hata hivyo Tottenham imesema itachunguza kwa kina juu ya kashfa hiyo kutoka kwa wanadinga wake.
  • Meneja wa Spurs Jose Mourinho alikubali kuwa alikiuka kanuni za kujitenga baada ya kuwa katika mazoezi madogo na kiungo wake aliyesajiliwa kutoka Lyon Tanguy Ndombele.
  • Wachezaji wa Arsenal Alexandre Lacazette, David Luiz, Nicolas Pepe na Granit Xhaka walivunja kanuni za kujitenga hasa kwa kuonekana katika picha iliyowaonyesha kukaa karibu karibu.
  • Kiungo mshambuliaji wa Chelsea Mason Mount alionekana katika picha ya pamoja na kiungo mkabaji wa West Ham United Declan Rice licha ya siku chache mchezaji mweza Callum Hudson Odoi aligundulika kuwa na Covid-19 ambapo alijitenga kwa siku 14.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends