Tottenham yamfurusha kocha Pochettino

Tottenham wamemtimua kocha mkuu Mauricio Pochettino baada ya kuwa usukani wa klabu hiyo ya Premier League kwa miaka mitano.

“Tulikuwa na wakati mgumu sana kufanya mabadiliko haya na sio uamuzi ambao Bodi imeuchukulia kwa urahisi, wala kwa haraka, amesema mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy.

“Tunajuta kuwa matokeo ya mechi za mashindano ya ndani mwishoni mwa msimu uliopita na mwanzoni mwa msimu huu yamekuwa mabaya sana.”

Kocha huyo wa zamani wa Southampton mwenye umri wa miaka 47, aliteuliwa Mei 2014 na kuiongoza Spurs hadi fainali ya Champions League msimu uliopita, ambapo walishindwa na Liverpool.

Spurs wamekuwa na mwanzo mbaya katika msimu huu na wako katika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends