Tour du Rwanda kuanza kutimua vumbi

Mashindano ya kila mwaka ya kuendesha baiskeli ya Tour de Rwanda, yanaanza Jumapili 23.02.2020.

Yatakuwa ni makala ya 12 ya mashindano haya ambayo yanatarajiwa kumalizika tarehe 1 mwezi Machi.

Mamia ya wakimbiza baikeli yataanzia jijini Kigali na kupitia Musanze,Muhanga miongini mwa maeneo mengine ya nchi hiyo.

Mwaka 2019, mshindi wa mashindano haya alikuwa ni Merhawi Kudusk utoka nchini Eritrea.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends