Township Rollers wa Botswana watua Dar kuvaana na Yanga

Mabingwa wa Botswana kwenye ligi kuu nchini humo Township Rollers wametua Tanzania mapema kujiwinda na mchezo dhidi ya Yanga mtanange wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa dimba la taifa jijini Dsm siku ya kesho Jumamosi kuanzia saa 12 jioni.
Katika hali isiyo ya kawaida baada ya kutua nchini, maswali mengi yameibuka baada ya kutotumia vitu vilivyoandaliwa na timu mwenyeji kwa maana ya maji na juisi, inaelezwa kukwepa hujuma ambazo zimekuwa zikifanyika.
Timu hiyo ikiwa na msafara wa watu 38 namba ambayo inajumuisha wachezaji, makocha na baadhi ya viongozi hao. Kikosi hicho kilitua jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA). Wametua Bongo wakitokea Afrika Kusini ambapo walipitia baada ya kutoka kwao Botswana walikokuwa wameweka kambi.
Township Rollers inakuwa mara ya pili kurudi nchini na kucheza na Yanga ambapo miaka mitatu nyuma ilicheza nayo katika hatua hii Yanga iliondolewa nje kwa ushindi wa goli 2-1 ugenini na nyumbani sare.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends