TPL yarejea kwa kishindo baada ya michuano ya kimataifa

158

Ligi kuu Tanzania bara itaendelea Alhamisi baada ya kusimama kwa wiki mbili kupisha michezo ya kimataifa ya timu za taifa mbalimbali katika kufuzu AFCON mwakani ambapo kutakuwa na michezo miwili.

Katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga, Yanga itakuwa ugenini kumenyana dhidi ya Mwadui FC majira ya saa kumi kamili, ambapo huo unakuwa mtanange wa kwanza kwa Yanga kucheza nje ya dimba la taifa.

Kwenye mchezo huo Yanga itamkosa Yondani na Kakolanya, Pato Ngonyani na Papy Tshishimbi wameshindwa kwenda hivyo safu yao ya ulinzi imepungua kwani hata Abdallah Shaibu ‘Ninja’ yupo na timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 23,”

Katika dimba la Azam Complex- Chamazi Azam itaikaribisha Ruvu Shooting. Kwenye mchezo huo Azam itamkosa mshambuliaji Donald Ngoma anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu ambapo kuna uwezekano mshambuliaji mpya Obrey Chirwa anaweza kuwa sehemu ya kikosi.

Msemaji wa Ruvu Shooting Masau Bwire amejinasibu kufanya vizuri katika mchezo huo. Hali kadhalika kwa Jaffar Idd naye amesema hana shaka na kikosi cha Azam.

Mchezo wa mwisho Azam ilishinda goli 1-0 dhidi ya Kagera Sugar wakati Ruvu Shooting ilipoteza kwa goli 4-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.

Ratiba inaonyesha kutakuwa na mtanange mmoja siku ya Ijumaa bingwa mtetezi Simba itawakaribisha “Wanapaluengo” Lipuli FC ambayo haijawa na matokeo mazuri katika michezo ya hivi karibuni.

Author: Bruce Amani