Trent Alexander-Arnold awachonganisha Klopp, Southgate England

Kocha mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema amepata mshtuko baada ya nyota wake Trent Alexender-Arnold kutojumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England kilichocheza mechi tatu za kufuzu Kombe la Dunia Qatar 2022.

Alexander-Arnold aliwekwa kando kwenye timu ya taifa ya England na hakuwa sehemu ya kikosi ambacho kilicheza mechi dhidi ya San Marino, Albania na Poland.

Klopp amesema kuwa bado hajaelewa maamuzi ya Kocha wa England, Gareth Sothgate kwa kumuweka kando beki huyo na badala yake kumchukua Kylian Walker wa Manchester City.

Kwa sasa beki huyo amekuwa kwenye wakati mgumu uwanjani ambapo alikuwa kwenye janga la Corona jambo ambalo lilimfanya Klopp asiulize kwa nini aliachwa kwenye kikosi cha timu ya England, Novemba pia alikuwa anasumbuliwa na majeraha lakini kwa sasa anaonekana kuwa yupo fiti.

“Nimeshangazwa namna ambavyo hajawa kwenye kikosi, sikuwa na mpango naye mkubwa katika msimu huu kwa kuwa niliamini kwamba angekuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa, ila ajabu ni kwamba hajawa kwenye hicho kikosi jambo ambalo nimeshangaa.

Liverpool inapitia wakati mgumu kwenye mechi nyingi za msimu huu kutokana na wachezaji wake wengi kuwa nje ya viwango pamoja na majeruhi.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares