Trent Alexander-Arnold nje ya Euro 2020 baada ya kuumia

Kisicho riziki hakiliki. Beki wa kulia wa Liverpool na timu ya taifa ya England Trent Alexander-Arnold ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa kufuatia kupata majeruhi kwenye mchezo wa kupasha misuli kuelekea michuano ya Euro 2020 dhidi ya Austria uliopigwa Jumatano.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, inatarajiwa kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki sita na atarejea viunga vya Anfield kwa ajili ya matibabu zaidi.
Hata hivyo, kocha wa England Gareth Southgate amesema hataongeza ingizo jipya kwenye kikosi hicho.
Alexander-Arnold alikuwa ni miongoni mwa mabeki wanne wa kulia wa England, wengine ni Reece James, Trippier wa Atletico Madrid na Walker wa Manchester City.
Mchezo wa kwanza England watacheza dhidi ya Croatia Juni 13 siku ya Jumapili.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares