Tshabalala, Bocco, Kapombe wamwaga wino Msimbazi

Uongozi wa Simba umekamilisha zoezi la kuwaongezea mikataba mipya wachezaji wake wanne ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea kipindi kirefu cha usajili cha dirisha la mwezi Juni.

Kupitia ukurasa rasmi wa klabu, Wachezaji ambao wamepewa kandarasi ya kutumika klabuni hapo ni nahodha John Raphael Bocco, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe na nahodha msaidizi Mohammed Hussein Tshabalala ambaye kandarasi yake ilibakiza miezi miwili.

Bocco ambaye ni mzawa wa kwanza kufunga mabao zaidi ya 100 ndani ya Ligi Kuu Bara mkataba wake ulikuwa unafika ukingoni msimu wa 2020/21 utakapomeguka.

Anakuwa mchezaji wa pili kutambulishwa rasmi kuongeza mkataba ndani ya Simba baada ya nahodha msaidizi Mohamed Hussein kuongeza dili lake.

Kwenye Ligi Kuu Bara, msimu huu Bocco ametupia mabao 10 na ana pasi mbili za mabao.

Wachezaji wote wamepewa mkataba wa mwaka mmoja.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares