Tuchel atetea ukame wa Timo Werner Chelsea na Ujerumani

Kocha mkuu wa Chelsea Thomas Tuchel amesema mchezaji wake Timo Werner inatakiwa aache kufikiria juu ya ukame wake wa kufunga magoli badala yake acheze kawaida ili kurudisha ubora wake.

Mshambuliaji huyo raia wa Ujerumani amefunga goli mbili pekee katika mechi 31 za Chelsea na Ujerumani, lakini pia juzi Jumatano alikosa nafasi ya wazi akiwa anakitumikia kikosi cha timu ya taifa mtanange uliomalizika kwa kipigo kwa Ujerumani dhidi ya Macedonia.

Tuchel amefananisha mawazo ya Werner juu ya kufunga magoli na namna ya kumshawishi mwanamke kukubali: anasema ni lazima kuwa mvumilivu kila siku unajaribu.

“Hata magoli yatakuja tu akiwa mvumilivu”.

Aliongeza kuwa “Usifikirie sana. Mimi ni rahisi kusema kwa sababu kila mmoja kwa hivi sasa anamnyoshea kidole, lakini ni changamoto ambayo hana budi kukabiliana nayo”.

Werner alijiunga na Chelsea akitokea nchini Ujerumani katika klabu ya RB Leipzig kwa kitita cha pauni milioni 47.5 mwezi Juni 2020, ambapo alifunga goli 34 katika mechi 45 msimu wa 2019/20.

Akiwa Chelsea rekodi yake amefunga goli 10 katika mechi 39, hajafunga goli tangia afunge kwenye ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Newcastle United Februari 15 mechi 10 bila goli ngazi ya klabu na taifa.

Tuchel alisema Werner ataanza kwenye mechi dhidi ya West Bromwich Albion Jumamosi na haijapoteza mchezo wowote chini ya kocha huyo, amefikisha mechi 14.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares