Tuchel azawadiwa mkataba mpya Chelsea mpaka 2024

Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel ameongeza kandarasi mpya ya kuendelea kukitumikia kikosi cha The Blues, sasa mkataba wake kukomea Juni 2024.

Tuchel, 47, mwanzoni aliingia makubaliano na mabosi wa Chelsea kwa mkataba wa miezi 18 pekee, kufuatia kuiwezesha Chelsea kushika nafasi ya nne kwenye msimamo wa EPL, kufika fainali ya Kombe la FA pamoja na kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mbele ya Manchester City, wameona ni bora kumpa mkataba mrefu zaidi.

Kocha huyo wa zamani wa Mainz, Borrusia Dortmund, na Paris St-Germain alichukua nafasi ya kocha Frank Lampard mwanzoni mwa mwezi Januari 2021.

“Kuna mambo mengi zaidi yanakuja, tunaangalia mbele katika mafanikio na malengo zaidi”, alisema Tuchel baada ya kumwaga wino.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares