Tusker FC Wabanwa na Nzoia Sugar KPL

30

Ligi Kuu nchini Kenya imefikia patamu kwenye mbio za kuwania ubingwa ambapo Tusker FC wamevutwa shati na Nzoia Sugar kwa sare ya bao 2-2 mchezo uliopigwa Jumapili dimba la Ruaraka.

Nzoia Sugar wameizuia Tusker kwenda karibu kabisa na timu kinara Kakamega Homeboyz ambapo sasa sare hiyo inafanya kuwa pengo la alama tatu baina ya klabu hizo mbili pale juu.

Kwenye mechi hiyo, nyota wa kitanzania Ibarahim Joshua alifunga bao moja kwa upande wa Tusker FC kabla ya bao hilo kusawazishwa na Nzoia Sugar kupitia kwa Joseph Mwangi.

Mchezo ukawa haujamalizika ambapo, Nzoia walichukua uongozi kwa kufunga bao la pili kupitia kwa Ian Karani hata hivyo dakika mbili mbele Tusker wakarudisha bao hilo kupitia kwa Ibrahim Joshua tena na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 2-2.

Kocha wa Tusker Robert Matano akizungumzia mchezo amesema kikosi chake kilikuwa na madhaifu katika namna ya kujilinda hasa eneo la ulinzi.

Ni matokeo mazuri kwa Kakamega Homeboyz ambao jana Jumamosi walitoa sare ya bao 1-1 na Gor Mahia.

Author: Bruce Amani