Tusker Yapigwa 1-0 na Nzoia Sugar

142

Tusker FC imekutana na mshituko wa kupoteza mchezo muhimu dhidi ya Nzoia Sugar katika Ligi Kuu nchini Kenya FKFPL mtanange uliochezwa uwanja wa Sudi, mjini Bungoma, Jumamosi.

Tusker wakiwa kwenye uhitaji wa ushindi ili wakae kileleni mwa msimamo wa Ligi walijikuta wakifungwa bao la mapema kwa njia ya penati lililowekwa kimiani na James Kibande.

Pamoja na kuwa na dakika nyingi za kujifikiria kwa Tusker lakini Nzoia Sugar walibaki kuwa imara na kulazimisha ushindi mwembamba wenye alama tatu na sasa wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa KPL.

Kufuatia matokeo hayo, Tusker wanabakia nafasi ya pili nyuma ya vinara Gor Mahia ambao walishinda bao 1-0 dhidi ya Police.

Author: Bruce Amani