Tutaendelea kupiga magoti hata kama mashabiki hawapendi – Southgate

Kocha wa kikosi cha England Gareth Southgate amesema wataendelea kupiga magoti mwanzoni mwa mchezo kwenye michuano ya Euro 2020 kama ishara ya kupinga vitendo vya ubaguzi wa rangi ambavyo vimekuwa vikifanywa licha ya mashabiki kuonekana kama wanazomea wachezaji wa Englandw
Mashabiki wa timu hiyo walikuwa wanawaczomea na kupiga kileleni wakati wachezaji wakiwa wanapiga magoti katika mchezo uliochezwa dimba la Riverside dhidi ya Austria siku ya Jumatano.
Kocha Southgate akizungumzia hali hiyo alisema “Kuna baadhi ya watu hawajui ujumbe gani tunauwasilisha tukifanya hivyo”.
Akizungumza siku ya Jumamosi kuelekea mtanange wa Jumapili wa Romania “Tuko imara kama timu, tutaendelea kupiga magoti hata kwenye Euro 2020”.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares