Tutazoea kuishi bila Lionel Messi – Rais wa La Liga Javier Tebas

Rais wa Ligi Kuu ya Uhispania La Liga Hispania Javier Tebas amesema yuko tayari kuona ligi hiyo ikiendelea bila uwepo wa staa wa Barcelona Lionel Messi. Tebas anayasema hayo ikiwa ni miezi kadhaa imepita tangu Lionel Messi kuwasilisha maombi ya kutaka kuondoka klabuni hapo kutokana na kile kilichotajwa kuwa hawaelewani na Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu ambaye hata hivyo alitangaza kujiuzuru Octoba.

Tebas anahitaji Messi kusalia ndani ya Hispania na acheze La Liga lakini anasema hata akiondoka tutazoea kuitazama bila uwepo wake.

“Tungependelea kumuona Messi anabakia La Liga lakini aliondoka Cristiano Ronaldo na Neymar Jr hatukuona tofauti yoyote”, tuko tayari.

Staa huyo raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 33 atakuwa kwenye dirisha la usajili katika majira yajayo ya usajili mwezi Juni huku Manchester City na Paris Saint Germain zikitajwa kuiwinda saini ya fowadi huyo.

Author: Asifiwe Mbembela