Uchaguzi Mkuu TFF wanoga, wagombea wagongana mlangoni kuchukua fomu

Baada ya Shirikisho la Kandanda Tanzania TFF kutangaza rasmi kuwa zoezi la uchukuaji wa fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya TFF kuanzia Leo Jumanne Juni 8 tayari majina matatu yamefika makao makuu ya Shirikisho hilo Karume, Ilala Jijini Dar es Salaam.

Mapema Leo, Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba, Swedi Mkwabi alifika Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kuchukua fomu ya kugombea Urais wa TFF.

Zoezi la utoaji fomu limeanza leo lakini tayari majina mawili yameshaingia kwenye kumbukumbu za wanaowania nafasi ya Urais, Evans .G. Mgeusa na Zehor Mohammed Haji ni moja wapo mbali na lile la Wallace Karia anayetetea kiti hicho.

Mwisho wa kuchukua fomu na kurejesha ni saa 10:00 Juni 12 mwaka huu, na uchaguzi ni Julai 7, 2021.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares