Uefa itachezwa hata mwezi wa tisa – Rais wa Uefa Ceferin

Ligi ya Mabingwa barani Ulaya na Ligi ya Europa zitafutwa endapo tu zitashindwa kuchezwa mpaka mwezi wa tisa na vipingamizi vikiendelea hivi. Maneno hayo yamesemwa na Rais wa Uefa Aleksander Ceferin leo Jumapili alipokuwa akijibu swali juu ya hatima ya ligi hizo Ulaya.

Mbali na hivyo Rais Ceferin amesema wanajaribu kuona kama itawezekana kuchezwa bila mashabiki kuliko kufuta michezo.

Michezo ya Uefa imesimamishwa kwa kipindi kisichojulikana huku virusi vya Corona navyo vikiendelea kugonga vichwa vya wataalamu mbalimbali dunia.

“Tutaangalia, kama mamlaka zitaturuhusu kucheza, basi tutacheza na zikigoma hatuwezi kucheza. Timu tano kutoka Uingereza zinashiriki mashindano ya Uefa ambapo Manchester City na Chelsea ziko katika hatua ya mtoano klabu bingwa na Manchester United, Wolves na rangers ya daraja la kwanza zinashiriki Uefa ndogo.

“Kiukweli hatujua mambo mengi,” alisema Rais huyo. “Tunasubili maendeleo ya janga hilo ya Corona duniani lakini zaidi tunaangalia barani Ulaya. “Bado itabakia muhimu kucheza mechi zilizosalia bila uwepo wa mashabiki na ukaonekana kwa TV kuliko kutofanyika kwa michezo hiyo. Watu wengi wanahitaji iwe hivyo na inaleta nguvu ya umoja wetu ambapo watu wanataka iwe Julai au Agosti”. Aliongeza Rais Caferin.

Fainali zote za Uefa ambazo zilipangwa kufanyika mwezi Mei kwa maana ya Ligi ya Mabingwa na Europa ligi zimefutwa kutokana na janga la virusi vya Corona, tarehe mpya bado hazitangazwa.

Author: Bruce Amani