UEFA kuanzisha mashindano mapya ya vilabu

Shirikisho la Soka barani Ulaya, UEFA limepanga kuanzisha michuano mingine ya ngazi ya klabu barani humo, ambapo inatarajiwa kuanza mwaka 2021.

Kwa sasa kuna mashindano mawili ya klabu barani humo ambayo ni Ligi ya mabingwa Ulaya – Champions League na ile ya Europa League

Mkuu wa kamati ya mashindano ya UEFA, Andrea Agnelli ametoa kauli hiyo katika mkutano wa muungano wa klabu za Ulaya uliofanyika katika Mji Mkuu wa Croatia, Zagreb.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends