Ufaransa washinda 1-0 kwa Bosnia-Herzegovina kuwania Kombe la Dunia Qatar 2022

379

Mshambuliaji wa klabu ya FC Barcelona Antoine Griezmann amefunga goli lake la pili katika mechi zake tatu za kufuzu Kombe la Dunia, goli ambalo limeipa alama tatu Ufaransa dhidi ya Bosnia- Herzegovina mtanange uliopigwa Jumatano.

Baada ya dakika 45 kumalizika kwa sare, filimbi ya ungwe ya pili ilikuwa furaha kwa Griezmann na taifa lake kufuatia kufunga goli kwa kichwa akimalizia mpira wa kiungo mshambuliaji Andrie Rabiot.

Ushindi huo unaifanya Ufaransa kukwea kileleni mwa msimamo wa Kundi D alama saba katika mechi tatu.

Hata hivyo, mlinda mlango wa Tottenham Hugo Lloris alifanya sevu nzuri sana kwenye mechi hiyo na kuisaidia Ufaransa kwa ujumla kuondoka na alama tatu muhimu.

Author: Asifiwe Mbembela