Uganda Cranes wapoteza 2-1 mbele ya Togo mchezo wa CHAN

243

Timu ya Taifa ya Uganda – The Cranes imepoteza mchezo wa kwanza hatua ya makundi ya Kombe la Mataifa Bingwa Afrika CHAN dhidi ya Togo kwa goli 2-1 mchezo uliokuwa mgumu na mzuri ukiwa na magoli ya aina yake pia.

Katika mchezo wa kwanza wa makundi Uganda walilazimishwa sare ya goli 0-0 dhidi ya majirani zao Rwanda – Amavubi Stars ambao nao katika mchezo wa mapema uliopigwa leo Ijumaa wametoa sare tasa na mabingwa watetezi Morocco.

Magoli yamefungwa na Paul Patrick Mbowa likiwa la kujifunga kwa mlinzi wa Uganda kabla ya Kyenune kusawazisha bao hilo kwa shuti kali lakini Yendoutie Richard Nane akashindilia kibano kwa The Cranes.

Matokeo hayo yanaifanya Uganda mpaka sasa wakiwa wamebakiza mchezo mmoja dhidi ya Morocco kushika mkia wakati Morocco wakiwa vinara kwa alama nne, Togo pointi tatu na Rwanda alama mbili baada ya sare mbili

Author: Bruce Amani